Avsnitt
-
Jinsi ya Kujiunga na Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania
-
Saknas det avsnitt?
-
Happy Mother's Day
-
Machi 12 kama leo, mwaka jana, nilitangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli. Kabla ya tangazo langu hilo, tayari kulikuwa na tetesi kadhaa kwamba afya ya kiongozi huyo ilikuwa tete. Hata hivyo, kwa kupitia vyanzo vyangu vya kuaminika, nilikuwa mtu wa kwanza kutangaza kifo hicho. Lakini madhila yaliyonikumba baada ya kuweka taarifa hiyo hadharani, sintoyasahau. Nilitukanwa, nililaaniwa, nilitishwa, na kwa hakika laiti hao waliokerwa wangeweza kunifikia, bila shaka muda huu ningekuwa marehemu. Hatimaye, siku tano baadaye, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan alitangaza kuwa kweli Magufuli amefariki. Nami ikawa ahueni kwangu. Baadhi ya walionitukana, walikuja kuniomba msamaha japo haikusaidia kitu. Hata hivyo nafarijika kwa kuwatumikia Watanzania ipasavyo na kuwa chanzo cha kuaminika cha habari mbalimbali.
-
Heri ya Mwaka Mpya 2022: Malengo 10 ya Mwaka mpya (New Year's Resolutions)
-
Maadhimisho ya #SikuYaAfyaYaAkiliDuniani: Uzoefu wangu binafsi na nyenzo zilizonisaidia
-
Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu #SikuMiaZaSamia: Alikotoka, Alipo Na Aendako
-
Mahojiano exclusive na mwanasoka wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao Mkami, anayechezea klabu ya Entag El Harby ya Misri na pia ni mchezaji wa timu yetu ya taifa, Taifa Stars. Katika mahojiano haya, Himid anaeleza safari yake katika soka, changamoto za soka la Tanzania na kimataifa, tofauti ya mazingira ya soka la Tanzania na soka la Misri, nini kifanyike kukwamua soka la Tanzania, na ushauri wake hasa kwa vijana akiwa kama role model wao - kwa vijana wanaotaka "kutoka" kupitia soka, na ushauri kwa vijana wengine wote katika sekta mbalimbali. Himid ni mmoja wa mabalozi wetu wanaosaidia sana kuitangaza Tanzania yetu kimataifa.
-
Katika mahojiano haya, Dokta Zakayo Mmbaga anaeleza kuhusu
👉 Jinsi kuuguliwa na nduguye kulivyomfanya atamani siku moja awe daktari, na hatimaye ikaja kuwa hivyo.
👉 Jinsi kusaidia kuhudumia mifugo kulivyompa uzoefu wa kwanza wa kuchoma sindano na kutibu vidonda, na kumtamanisha zaidi kuja kuwa daktari.
👉 Jinsi alivyorudi likizo na kukuta nduguye anaumwa kansa lakini ndugu wengine hawakufahamu na wakawa na matumiani kuwa mgonjwa atapona lakini yeye kama daktari mwanafunzi alifahamu kuwa mgonjwa huyo angefariki. Hata hivyo hakuweza kumwambia mtu yeyote, kitu ambacho kilimuumiza nafsini.
👉 Jinsi gharama kubwa wanayoingia madaktari wanafunzi zinavyowafanya kuendelea kuwa na madeni yasiyolipika, huku jaribio la kujiendeleza kitaaluma likimaanisha madeni zaidi.
👉 Jinsi mazingira magumu ya kazi yanavyofanya taaluma ya utabibu kuwa ngumu, hasa pale inapolazimika kumuelekeza mgonjwa aende hospitali ya rufaa ilhali uwezo wake kifedha ni mdogo.
Kwa hakika mahojiano haya yanahamasisha, yanatafakarisha na yanasikitisha.
-
Katika mahojiano haya, mwanasiasa mkongwe wa Chadema na upinzani kwa ujumla, Ally Bananga, anaeleza kwa kifupi
👉 historia yake kisiasa,
👉 hali ya kisiasa ilivyokuwa nchini Tanzania katika kipindi cha utawala wa Magufuli na jinsi "alivyosalimika," 👉suala la wabunge wa viti maalum wa Chadema ambapo mmoja wa wabunge hao ni Hawa Bananga mke wa mhojiwa,
👉 "vita" kati ya baadhi ya "wanaharakati wa mtandaoni" wakiungwa mkono na viongozi na wafuasi wa Chadema dhidi msanii Diamond Platnumz anayewania tuzo za BET,
👉 utawala mpya wa Mama Samia na matajio, na
👉njia mwafaka ya kupata katiba mpya -
Mwelekeo Mpya Wa Podcast Hii: Sasa Mtu Yeyote Anayehitaji Kuhojiwa, Anakaribishwa
- Visa fler